3.4. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Nne - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Feb 14, 2016, 3:23 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Siasa hasa ni nini? Wakenya wengi wamepotoka na kufikiri siasa ni kufurahia vya bwerere kila baada ya miaka mitano uchaguzi mkuu unapotangazwa. Siasa ni utaratibu na maadili yafaayo. Siasa bora chambirecho Rais Mstaafu, ni maisha bora. Wakenya wakitafuta siasa zilizokomaa bila shaka tutafurahia matunda yake.
Matunda matamu ya siasa ni kama uimalishaji wa elimu, shuguli za afya, barabara, usalama na haki ya utulivu katika nchi. Kinyume cha haya, siasa mbaya huzusha uhasama, umaskini na machafuko ya maisha kwa jumla kwa wakenya. Sasa swali ni hili: tulipo shiriki uchaguzi, je tuliwachagua viongozi wenye vipawa vya uongozi walielekeza jahazi letu fanakani au tunajua kuchagua mabwanyenye wafisadi watakao lizamisha jahazi letu?
Haki ya mwanchi katika siasa za nchi yake ni zipi? Bila shaka ni kutumia kula yake kuchagua mwakilishi anayefaa ili kusaidia kutunga sheria nzuri bungeni zitakazo ongoza shughuli za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa manifaa ya wakenya.
Jambo lingine muhimu wakati wa kampeni ni kundumisha amani na kutofuata uandui wa vyama mbalimbali vya kisiasa. Watakaoimbuka washindi washughulikie nchi yao, yaani waeke mbele maslahi ya wananchi na sio mahitaji ya binafsi.

1. Wananchi wanafaa washiriki katika siasa za nchi yao kwa _____________
a. kuwachagua viongozi wao.
b. kujiburudisha wakati wa uchaguzi.
c. kuongoza jahazi letu.
d. kuchagua mabwenyenye bungeni.
2. wananchi wanaharibu siasa za nchi kwa
a. kutunga sheria zisizofaa
b. kujiunga na vyama vya kisiasa
c. kukumbali kuhongwa na wagombea uchaguzi
d. kutawala bila haki
3. Kati ya haya yafuatayo ni lipi lisilo tunda la siasa
a. Afya bora
b. ujenzi wa baraste
c. vurugu
d. utulivu
4. Jahazi lililotajwa katika ufahamu ni__________
a. meli
b. wafisadi na watenda haki serikalini
c. vipawa vya uongozi
d. maisha ya maendeleo kwa wananchi
5. Neno zilizokomaa limetumika katika habari hii kumaanisha
a. zilizofika mwisho
b. zilizoimarika na kufika kiwango cha juu
c. kuanzisha jambo
d. kutoa kitu kilichokwama
6. Neno hongo lina maana sawa na__________
a. chai
b. riba
c. mchango
d. hongera
7. Mwakilishi wa nchi katika baraza la taifa la kutunga sheria ni___________
a. diwani
b. wakili
c. mbunge
d. balozi
8. Wawakilishi wengine wa wananchi hukosea kwa
a. kupinga maendeleo na kutenda haki
b. kupokea hongo
c. kuyaweka maslahi yao mbele
d. kukosa vipawa
9. Chagua sentensi sahihi kulingana na habari hii
a. siasa bora huleta ustawi nchini
b. matajiri pekee ndio wafaao mbungeni pekee
c. matunda ya siasa bora ni uhasama
d. vyama vingine vya kisiasa
10. Kichwa kifaacho zaidi habari hii ni
a. vyama vingi vya siasa
b. siasa bora
c. uchaguzi
d. amani na upendo

kiswahili revision papers