3.5. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Tano - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 2:50 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Bwana mmoja mtana shati, mfuaji na mlibwende sana, alioa mke nadhifu, mrembo na maridadi zaidi. Baada ya siku kadhaa ndoa ikaingia doa. Wakawa hawasemezani wala hawaongeleshani. Cheko na bashasha zao zikayeyuka kama mawingu ya jangwani.
Bwana akitoka kazini, kimya cha kaburi. Bibie naye kanuna kando- watani husema kauma jongoo. Au kanuna kama shetani.
Siku moja bwana alitoka matembezini. Alichoka sana. Saa nane baada ya kishuka aliamua kujipumzisha kidogo kitandani akisubiri saa kumi na mbili aingie kazini shifti au zamu ya usiku. Alijua usingizi ungemwiba na huenda akalala fofofo achelewe kwenda kazini. Lakini afanyanje ilhali yeye na mke wake hasemezani. Potelea mbali! Liwalo na liwe!
Akatwaa kipnde cha karatasi akaandika;”Mke wangu zikifika saa kumi na saa kumi na nusu uniamshe niende kazini.” Kikaratasi hicho chenye urafa, akakitupa mbali bila kukikunja njuu ya meza.Akaenda kititandani na kujibwaga.
Mke alipoenda ukumbini,akakisoma. Mnh! Naam, ilipofika saa kumi na moja unusu, mkewe mtu naye akatwaa kipande cha karatasi na kuandika,”Mume wangu, saa kumi na moja unusu zimetimuia, amka uende kazini.”
Yule bwana aliupata usingizi wa pono. Akalala fofofo mpaka saa moja jioni. Kachelewa kazini tayali alipoamka, nikwambie nini? Sijui tu. Labda wewe uniambie. Je kosa la nani?

1. Habari hii inatuarifu kwamba___________
a. watu maridadi wakioana huishi maisha ya taabu.
b. mwanamke mrembo huwa na doa.
c. bwana na bibi huyo walionana kwasababu ya urembo.
d. arusi ya watu hawa ilikuwa ya kukata na shoka.
2. Ndoa yao iliingia doa. Yaani
a. Ilivunjika
b. Ilipata ila
c. Iliharibika
d. Iliyeyuka
3. Baada ya ndoa kupata doa, waliishi_________
a. vizuri.
b. kama maji na mafuta.
c. kama chai na mbizi.
d. kama ardhi na mbingu.
4. Bwana alipotoka matembezi, alikuwa na masaibu yapi?
a. Uchovu
b. Usingizi
c. Njaa
d. Ukinya
5. Bwana alienda kulala baada ya kufanya nini?
a. Kuandika arafa.
b. Kula chakula cha adhuhuri.
c. Kula chajio.
d. Kuwaza na kuwazua mbinu za kuwasiliana na mkewe.
6. “potelea mbali! Liwalo na liwe!” Kwa neno moja ni___________
a. sijali
b. haidhuru
c. sikitu
d. usikujali
7. Mke naye alipoandika kwenye karatasi, alikuwa
a. akidhahaki mumewe.
b. akimwasha.
c. akilipiza kisasi.
d. akimpenda.
8. Neno arafa lina maana ya___________
a. makala
b. ujumbe
c. nyaraka
d. taarifa
9. Kinyume cha usingizi wa pono ni usingizi wa
a. shinda
b. mang’amung’amu
c. upesi
d. fofofo
10. Habari hii ni juu __________
a. umuhimu wa mawasiliano.
b. umuhimu wa mapenzi nyumbani.
c. hasara za ndoa. kuvunja ndoa.
d. Kuvunja ndoa

kiswahili revision papers