3.6. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Sita - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 9:45 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Kinchonikera na kunikereketa ni kitovu cha kimya chako au labda umeghafilika kuwa kina mshindo?hata
Hivyo, ninayo imani kuwa kimya hicho si cha hujuma wala tuhuma ,ila shuguli zilizokubana.
Natumaini mwaka unaozidi kutupungia mkono wa buriani umekuwa wenye fanaka kwako. Natarajia kwa
Kuangukiwa na kikuti kibichi ulivyonidekezea umeti bidii kabamke . Kumbuka sana kuwa mgaagaa na upwa hali wali mkavu
Baba yangu anayo matumaini mengi kwamba tutajiunga na wenzetu tuliopendana nao kama chanda na pete hapo mwakani katika shule ya upili.
Yatategemea matokeo ya mitihani ambayo ninayasubiri kwa hamu na raghba kama ya mkanja.
Umbu yangu mkubwa ambaye ndiye mwanambee ameniahidi zawadi muru endapo matokeo yatakuwa ya kufana.Mimi ninayo hakika kama mauti ,kazi zote tulizozifanya kama maandalizi kabla ya mithani hazitaambulia patupu chambilicho mwalimu wetu kisawhili Bwa. Lisao,kinolewacho bila shaka hupata.
Naam Adhia ningependa kukualika kwetu tarehe 30.12.2010 . Tutakuwa na dhifa katika zile pilka pilka na shamra shaamra za kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya . Naomba kwa hiari yako usikose na uje na kina sankate na staki kwani iliyo lakabu yake ,kila moja na nusu ya nyama ya ndovu ni kwa raha zake.
Nilikikunja jamvi na kuuokoa wino unaoelekea kwisha ilhali unaadimika kama barafu ya kukaanga ,na kutakia wewe rehema za kahari. Hadi tutakapoonana tarehe 30.12.2010.
Naliomba kukuona hapa.
Wako wa dhiki faraja.

1. Mwandishi anamkirimu mwenziwe kwenye dhifa ya nin?
a. Siku kuu
b. Harusi
c. Kibuhuti
d. Siku ya kufunga
2. Mwandishi wa barua hili hasa amekuwa katika rajua ya
a. Darasa la nane
b. Kidato cha kwanza
c. Chuo kikuu
d. Kazi ya udaktari
3. Waraka wa sampuli hii ni aina gani?
a. Kindugu
b. Kidugu
c. Rasmi
d. akilimali
4. ________ilivyo lakabu yake___maana ya maneno hayo ni ____
a. Jina la mwandishi
b. Jina la mzimbo
c. Jina la mwanafunzi
d. Jina la shuleni
5. Waraka huu uliandikwa lini?
a. Muhula wa kwanza
b. Mwezi wa krismasi
c. Likizo ya disemba
d. Likizo yz muhula wa kwanza
6. Taksiri ya barua hii ni______
a. Anwani
b. Jina la mwandishi
c. Jina la mwandikiwa
d. Sahihi ya mwandishi
7. Kwa mintaarafu ya methali ,kinolewacho hupata,mwandishi anamwona,mwalimu akishabihi nani?
a. Sonara
b. Msembe
c. Muhuzi
d. mjumu
8. yamkini mwalimu lisao anafunza somo lipi
a. kiingereza
b. hisabati
c. Kiswahili
d. Sayansi
9. Baba yake mwandishi ana matumaini kuwa mwandishi na rafikiye watajumuika na masahibu wao japo yote yatategemea___
a. Visala
b. Bahati
c. Natija
d. mitihani
10. umbu yake mwandishi ndiye mwanambee ilihali mwandishi ni_____ wake.
a. Mlungizi
b. Mziwanda
c. Mlanguzi
d. mkadamu

kiswahili revision papers