3.7. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Saba - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 9:58 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Bara la Afrika kwa miaka mingi ni eneo ambalo limekumbwa na misukosuko. La kila aina, mojawapo ikiwa ni tatizo sugu la ukabilia. Ukabila ni dhana ambayo inachochea michemko mikali ikizingatiawa kuwa ukabila na rushwa ndivyo visingiti vikubwa vya maendeleo katika bara la Afrika.
Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya lugha , siasa na ukabila hivi kwamba mwanasiasa hutumia lugha kuelezea sera isiyo na yake hasa wakati wa kampeini ya kuomba kura. Lli kuwashawishi watu wasio wa kabila lake, hana budi kuitumia lugha isiyo na hisia za kikabila katika bara la Afrika, bara ambalo lina wingi wa lugha ya Kiswahili inaweza kuwa lugha ya kuondoa dondadugu la ukabila ambao umeathiri katika hili lakini sio Kiswahili chochote tu kinachoweza kutimiza wajibu huu. Ni Kiswahili ambacho katika matamshi ya wazungumzaji hakitabainisha wanatoka katika kabila lipi.
Mara kwa mara unapo wasikiliza watu wakiongea kwa Kiswahili, unaweza kubainisha wao ni watu wa kutoka meru,kisii,ukambani,wakalenji,wadigo au wengine. Msomi mtaji Kiswahili mnamo mwaka jana katika karatasi kongomano la chakita mjini nyahururu, alitoa kauli kuwa wakenya ni maadui wa Kiswahili kwa sababu wengine wameshindwa.

1. Mbona mwandishi anasema eti ukabila ni tatizo sugu?
a. Halisikii dawa
b. Limekwepa matibabu
c. Wakabila ni watu
d. Unaangamiza watu wengi
2. Mambo mawili ambayo yanaaminika kuwa na uhusiano wa karibu na lugha ni
a. Siasa na ukabila
b. Afrika na Rwanda
c. Dini na siasa
d. Wameru,wakisii na wadigo
3. Ni Kiswahili kipi kitaangamiza ukabila?
a. Kilicho na msamiati mwafaka
b. Kisicho na lahaja ya lugha mama
c. Kisicho na uegemeaji wa vitabu
d. Cha tanzania
4. Unadhani wa Kiswahili unajidhihirisha mno kwa mujibu wa____
a. Mavazi
b. Chakula
c. Lafudhi
d. itikadi
5. kwa mintaraafu ya habari ,vizuizi vikubwa vya maendeleo vilivyotajwa ni pamoja na____
a. nchi ya taifa
b. wadigo na wakisii
c. chuki na uadui
d. ukabila na wameru
6. kwa maoni ya mwandishi , ni lipi ndilo dondadugu Afrika?
a. Kiswahili
b. Lugha
c. Ukabila
d. makabila
7. mwanasiasa anahitaji lugha isiyo na hisia za kikabila ili
a. kutumiza ndoto yake
b. kufanya kampeni
c. kufafanua sera zake
d. kupiga siasa
8. aliyesema eti wakenya ni maadui wa Kiswahili alikuwa akifanya nini?
a. Akisoma
b. Akihutubu
c. Akitibu
d. akichangia
9. kongomano linalotajwa lilifanyiwa katika mji gani?
a. Chakita
b. Nairobi
c. Nyahururu
d. mashariki
10. Anwani aula kwa habari uliyoisoma itafaa kuwa?
a. Kiswahili Afrika
b. Lugha ya Kiswahili
c. Ukabila katika Kiswahili
d. Matatizo ya Kiswahili.

kiswahili revision papers