3.8. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Nane - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 10:11 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


“Afanaleki Makeke ajibaza kando ya gurufu, kwani yeye ni kiruu?” Mpita njia mmoja akajiuliza Yakini chambilecho wahenga “kuna malimwengu ulimwenguni” muda si kiduchu. Shogaye makeke akatoke mkabaia wa tukio huku akienda masia kando ya baraste, akiandamana na auladi wake.
Makeke kwa kumwona shogaye, aliita kwa sauti,Mhisani wangu njoo nafaa. Shogaye kwa kusiku sauti ya mjaanayembaini. Malaika yalimsisimka. Alitembea guu mosi guu pili, lama mahali pa mkasa kwani mtu hakatai mwito bali aitwalo.
Alipofika mahali pa mkasa, alimkuta Makeke si hayati si mamati. Alipomuuliza ni yapi yaliyo jiri Alimdokezea kuwa aligubia mvinyo juzi si haba. Alifanya ima fa ima kuitisha daladala na kumpeleka hospitalini. Ibura ni kwamba , alifarakana na sayari ya tatu kabla ya kutibiwa. Hapo ndipo nilipo sadiki kuwa msiba wa kujitakia hauna kilio.

1. Makeke alijibanza wapi
a. Kwenye kiruu
b. Barabarani
c. Hamamuni
d. Kando ya mti mkubwa
2. Afanaleki ni mbinu gani ya kisanaa?
a. Kivumishi cha sifa
b. Kiulizi
c. Kihusishi
d. kihisishi
3. makeke alikuwa wa jinsa gani?
a. Kiume
b. Kizee
c. Kike
d. mkembe
4. Ni jambo gani lililomfanya Makeke kujibanza kando ya gurufu?
a. Kuvaa miwani
b. Kupigwa kago
c. Kufa ganzi
d. Kutiwa mbaroni
5. Mtu kiruu ni mtu wa aina gani?
a. Mtevi sana
b. Mkata wakiasi
c. Mchochote
d. Kukosa akilitimamu
6. Mtu anapopewa jina kulingana na hulka zake huitwa?
a. Lakabu
b. Majazi
c. Sadfa
d. tanakani
7. Si hayati si mamati, Hii ni mbinu gani ya usani?
a. Wasifu
b. Shada
c. Istiara
d. tashbihi
8. Eleza maana ya nahau “Malaika yalinisisimka.”
a. Kushangaa
b. Kuwa na kiwewe
c. Malaika kumtoka
d. Mwili kufa ganzi
9. Sayari ya tatu huitwa?
a. Utaridi
b. Kausi
c. Zaibaki
d. Dunia
10. Shogaye Makeke aliandamana na _____
a. Msichana wake
b. Mume wake
c. Mvulana wake
d. Mkoi wake

kiswahili revision papers