3.9. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Tisa - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 10:29 PM ]

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali 1-10


1. Twajitoa hadharani, kusema
Juu ya haki duniani, kwa wamama jamani
Wazi twaelele, kwa maneno vikaoni
Akina mama amkeni, gubigubi mwafunikwa
2. msifunikwe yakini, enyi mama amkeni
Vibwebwe jitungeni, zenu haki zidaini
Rudi nyuma asilani, mbele ndiko safarini
Akina mama amkeni, gubigubi mwafunikwa
3. Haki hizi haki gani? Za wamama kudaeni
Peupe taelezeni, kwa maneno vikaoni
Kwanza usawa daeni, kotekote nyanjani
Akina mama amkeni, gubigubi mwafunikwa
4. Taasuhi za zaani, mke kwake jikoni
Na zizikwe baharini, la sahau hizo imani
Imaima fanyeni, mkwepe hizo imani
Akina mama amkeni, gubigubi mwafunikwa
5. saasani ingieni, bungeni piganieni
Mamlaka gobeeni, katika serikalini
Mhanga jitoeni, tafanikiwa amani
Akina mama amkeni, gubigubi mwafunikwa
6. Uchumi jitieni, rasilimani wekeni
Biashara anzeni,kotekote nchini
Pesa nazo chumeni, imarika uchumini
Akina mama amkeni, gubigubi mwafunikwa
7. Beti saba ukingoni, shairi kaditamani
Haki zidumisheni, kwa wamama ee!!! Jamani
Ubaguzi epukeni, kazi na mamlaka
Akina mama amkeni, gubigubi mwafunikwa

1. Taja bahari ya shairi hii
a. Tamthinia
b. Tarbia
c. Ukumi
d. utao
2. malenga ametumia kielezi kipi katika mkarara
a. kifani
b. tashbihi
c. tanakali
d. wakati
3. Taja kisawe cha usemi kujifunga vibwebwe
a. Kujigunga madombo
b. Kuja yamini
c. Kujifunga kamka
d. Kujifunga udodi
4. Tambua mleo wa ukwapi katika ubeti wa pili
a. Zenu hadi zidaeni
b. Msifunikwe yakini
c. Rudi nyuma asilani
d. Mbele ndiko safarini
5. Kipande cha tatu katika shairi huitwa____
a. Kikwamba
b. Urari
c. Mwandamizi
d. ukara
6. taja ujumbe wa mshairi katika ubeti wa tano
a. akina mama waingie siasani
b. akina mama wasiingie siasani
c. wawe wazembe
d. katu wasiwe wabunge
7. mshororo wa pili katika mwanzo wa ubeti wa tatu
a. molto
b. kituo
c. mleo
d. ubeti
8. tambua mizani katika mwanzo wa ubeti wa tatu
a. 5
b. 18
c. 16
d. 14
9. Mwenye kutunga mashairi na kuimba huitwa?
a. Malenga
b. Mkariri
c. Manju
d. mkutubu
10. kichwa mwafaka kwa shairi hii ni______
a. usawa
b. akina mama amkeni
c. taasubi za kale
d. siasa

kiswahili revision papers