4.1. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Nne Sehemu ya Kwanza - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 28, 2015, 12:01 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Hauchi hauchi hucha.Hatimaye siku tuliokuwa tukisubiri iliwadia .Kijiji kizima kilikuwa kikisubiri matukio ya siku ile kwa hamu kubwa .Unaweza kusema maisha ya baadaye ya kijiji au hatima ya kijiji chetu ilitegemea siku hiyo .sote tulikuwa ange kulijua mbichi na mbivu .Kupembua mambo na kuyaweka bayana kwa kila mmoja ayaone waziwazi.
Kwa miezi kadhaa iliyopita,wananchi waliishi roho –mkononi.Suala la usalama kijijini lilikuwa kama kitanzi kilichotishia kuinyonga sio tu roho ya kila mwanakijiji bali kijiji kizima.Mwanzoni,mwanakijiji walilalamika kuwa lilikuwa tatizo la upetevu au zohali ya wanaohusika na usalama.Haikupita siku bila ya kusikia visa vya kutikisha kuhusu uvamizi kijijini.Mwanzoni watu walipuuza kwa kusema kuwa lilikuwa tatizo la muda;wingu la kupita tu.Lakini matatizo hayo yalirudufika na wanakijiji kuanza kushikwa na hofu kubwa.Hatimaye yalikuwa ya kila uchao.
Watu waliamua kuunda vikundi vidogovidogo ili kuikabili hali yao mpya .kwa muda mambo yalibadilika.Watu walishusha pumzi kwa siku kadhaa lakini kama volkeno iliyokuwa imetulia ,wahalifu walivuvumika tena. Ulikuwa wakati huu watu walipoamua kuandika barua kwa mkuu wa wilaya .Naye hakukawia kujibu barua hiyo na kutenga siku ya kuja kukutana na wanakijiji wenyewe.Hii ndiyo iliyokuwa siku muhimu.
Uwanja mzima ulitapika watu na kuwafurika wengine mbali huko.Kila mmoja alitaka kuwepo na kushiriki katika maamuzi hayo muhimu .Mkuu wa wilaya aliwasili saa nne kamili.Watu waliokuwa wameteuliwa kuzungumza walizungumzia kuhusu dhiki na karaha iliyowakumba watu.Walikuwa watu wa kila umri na kufu;kuanzia vijana hadi wazee ,hamna aliyebaguliwa .”Ndugu mkuu wa wilaya , tunahiliki hasa majanga si majanga haya .Kila siku uvamizi ndiyo huo .vitu vinaibiwa.watu wanapigwa kabali.wanawake wanabughudhiwa.Kero si kero hii.
Mkuu wa wilaya alisikiliza kwa makini .Baadaye aliwataka watu kutoa mapendekezo yao ,jinsi ambavyo usalama wa pale ungedumishwa .Mwishowe ilikubaliwa kuwa doria za polisi zingeongezwa .Ilianzishwa kamati ya wazee ya kuhakikisha kuwa wanakijiji walihusiana na polisi vizuri bila ya tuhuma wala hofu yoyote.Uliundwa utaratibu mzuri wa kuwasilisha taarifa kwa polisi bila ya kuwapo na hofu ya kujulikana na wahalifu waliohusika .Wanakijiji walitwaa jukumu la kuelimishana kuhusu usalama wao.
Jioni walipokuwa walifumukana kuenda makwao ,kila mtu alitumaini kuwa kuchwa kwa jua siku kuliashiria mwisho wa maovu kijijini .Wote walikuwa na matumaini makubwa .kila mmoja wao alikuwa ameapa kuwa angejitolea sabili,hali u mali kuhakikisha kuwa maisha ya kijijini yalichukua mkondo mwingine .Ndivyo ilivyokuwa .Ushirikiano wa wanakijiji na serikali uliishia kubadilisha hali kijijini .Siku hiyo ikabakia siku ya kukumbkwa na kila mwanakijiji.

1. Yupi si mdudu kulingana na aya ya kwanza?
a. Mende
b. Buibui
c. Kipepeo
d. Panzi
2. Maelezo yapi ni kweli kuhusu wadudu?
a. Wadudu wengi hawana hadhara
b. Wadudu wote wanajulikana
c. Wadudu wanaojulikana si wote
d. Wadudu wanaojulikana si wengi
3. Kuhusu mbu ,mbung`o na mende na kunguni.
a. Wote ni vimelea
b. Wote si vimelea
c. Wote hawana madhara
d. Wote hawana manufaa
4. Chagua orodha ambayo si sahihi
a. Mbung`o,kichocho
b. Nzi,tauni
c. Mende ,kipindupindu
d. Nzi,kipindupindu
5. Mbung`o ni mdudu hatari kwa vile
a. Huathiri na hata kufisha mifugo
b. Huua karibu nusu ya mifugo barani Afrika
c. Huathiri mifugo na binadamu pia
d. Huua watu wengi hata kuliko mifugo
6. Nzige ni tishio kubwa kwa nchi yoyote kwa sababu
a. Husafiri katika makundi makubwa sana
b. Huweza kusababisha baa la njaa
c. Huleta madhara mengi kuleta wadudu wote
d. Huogopwa zaidi ya wadudu wote
7. Uhusiano uliopo baina ya nyuki na kipepeo na nyuki ni kuwa
a. Wote hutupatia asali n anta
b. Wote ni wadudu wanaoleta maafa
c. Ni wadudu maridadi wanaovutia sana
d. Ni wadudu wanaoeneza mbwelele
8. Jina jingine la mende ni
a. Nyenje
b. Komba mwiko
c. Parare
d. Ndorobo
9. Msimamo wa mwandishi wa makala haya ni kuwa
a. Kuhifadhi kwa mazingira kunaweza kuimarisha uchumi
b. Kutunza usafi kunaweza kuwaangamiza wadudu wote
c. Kutumia dawa ni njia bora zaidi ya kuwaondoa wadudu
d. Kufuga vivunjanjugu kutatuondolea vimelea hatari
10. Mtu yupi anaweza kufananishwa na kupe kwa mujibu wa makala
a. Asiyependa kufanya lolote ila kupumzika
b. Mchafu asiyeoga ila kwa nadra sana
c. Mharibifu anayewaletea wengine hasara
d. Mlegevu apendaye kuwategemea wengine

kiswahili revision papers