4.2. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Nne Sehemu ya Pili - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 29, 2015, 9:18 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Ajira ya watoto ni suala linalovutia wahisani wa nchi nyingi kote ulimwenguni.Utafiti kuwa watoto wengi umeonyesha wamedhulumiwa kupita ajira ya watoto.Hapa nchini Kenya ,watoto wanaoajikuta katika hali hii ni watoto ambao ni mayatima au wazazi wasioajibika pamoja na watotoambao aidha walikosa kuendelea na shul e baada ya darasa la nane au hawakufika darasa la nane.
Ni dhahiri shahiri kuwa baadhi ya watoto wanaotaka katika jamii maskini hutumiwa na wazazi ili kuleta mapato zaidi nyumbani .Watoto hawa wakati mwingi hulazimika kuajiriwa kama wasaidizi mashambani kuchuna kahawa majani chai,nyumbani ,uvuvini,kuuza vinyago na kwenye migodi na katika jamii za kuhamahama watoto wengi hawapelekwi shuleni mbali hutumiwa na wazazi kutunza mifugo na pia kuajiriwa kwa kazi iyo hiyo.
Aghalabu chanzo cha ajira ya watoto ni ustawi na viwanda. Katika karne ya kumi na nane huko uropa,ustawi wa viwanda ulipoanza watoto wa miaka minane waliajiriwa kufungua na kufunga milango ya viwanda kila watu wanapopita ama mizigo inapoingizwa na kutolewa viwandani.Nchini Kenya shuguli za ukulima kwa mapato na vitega uchumi vimechangia ajira za watoto.
Ni vyema kufahamu kuwa ili suala la ajira lidhihirike maishani mwa binadamu yeyote ni lazima kukumbuka kuwa watoto hawa huwa hawajamiza umri wa kufanya kazi na wakkati huu huwa wanapaswa kuwa shuleni wakikua kihisia,kimawazo na hata kimaumbile.

1. Swala la ajira ya watoto limevutia____ wa nchi nyingi kote ulimwenguni.
a. Watu wa maabada
b. Watu wote
c. Watu wenye kutenda mema
d. Matajiri na maskini
2. Utafiti umeonyeshakuwa watoto wengi____kupitia kwa ajiri ya watoto
a. Wamenufaika
b. Wamedharauriwa
c. Wamenyanyaswa
d. wamesaidiwa
3. watoto hawa katika nchi ya Kenya hupatwa naaa hili jinamizi la ajira.Ni ganihawahusiki?
a. Watoto wa matajiri
b. Watoto wa wazazi wasiowajibika
c. Watoto wa mayatima
d. Watoto walioacha shule
4. Badala ya kusema dhahiri shahiri tunaweza sema ____
a. Fauka ya
b. Bayana
c. Upungufu
d. Moja kwa moja
5. Watoto wanaweza,kupata ajira kupitia kwa njia hizi ila___
a. Kuvuna kahawa
b. Kuvuna majani chai
c. Kazi ya nyumbani
d. Kuenda shuleni
6. Watoto wa wafugaji hawapelekwi shuleni kwa nini?
a. Kwa ajili ya kuhamahama
b. Hawapendi shule
c. Umaskini
d. Mali wanayo imiliki
7. Neon aghalabu lina maana___
a. Fauka
b. Saidi
c. Minghairi
d. Mara nyingi
8. Neon uropa limetumiwa kumaanisha
a. Kaunti
b. mpira
c. Nchi
d. bara
9. kati ya hawa ni yupi ambaye akipatiwa kazi ni ajira kwa watoto?
a. Miaka ishirini
b. Miaka thelathini
c. Miaka kumi mna sita
d. Miaka hamsini
10. Kichwa mwafaka cha habari hii ni___
a. Watoto
b. majira
c. ajira ya watoto
d. Kenya na mayatima.

kiswahili revision papers