4.5. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Nne Sehemu ya Tano - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Aug 3, 2015, 9:34 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Babake Mwaipaasa alikuwa akivuta pumzi zaka za mwisho akiwa kitandani. Alikuwa hoi bin Tiki. Mabebe yalimtoka akabaki gofu la mtu.Alikuwa dhaifu kama utumbo wa samaki yaani mchege kalegea .Kwa sauti tetemesha alimwita mwanawe na kumwashiria akae mfumbati wa kitanda chake ingawa ilikuwa mwiko. Lakini wenye ndimi za wahenga walisema lisilobudi hutendwa. Mzee alikuwa hasimani hasongiu . Ugonjwa ulimlaukamguguna kama mchwa kwenye Shushu. Akafumbua mdomo kwa shida na dhiki, akamwambia Mwaipasa, “Mwaipasa, Sasa hivi unavyoniona dau langu, linakaribia ukingoni. Nina yako hayupo, nami nafuata Njia ile unyounyo. Unaelewa fika nduli huyu asiye na dawa wala kafara.Na kwa kuwa wewe ndiwe Mwanambee una jukumu la kuwelea ndugu ako. Pia nakusihi uzingatie elimu hata Kichele kwani ni taa iangazayo gizani. Mali huisha jinsi ulivyoshuhudia. Sasa sisi
ni maskini nasi hatuna be wala te, japo tulikuwa matajiri wa kutajika. Kumbuka kuwa kisomo ni zana aula ya kuangamiza umaskini, ujinga na upofu wa maisha. Ushikilie uzi wa masomo kikiki.Kama kupe kwenye mkia wa ngombe . “Naapa kufanya Hivyo baba”, alijibu. Baada ya baba yake kumtolea Vito vya maneno, hakuchukua muda Mrefuhalafu akakata kamba. Mwaipasa pamoja na ndugu zake sita wakabaki mayatima. Baada ya maziko ukweli ukamjia Mwaipasa Wanuna wake wakawandiye wanayemtegemea Ili vikono viende vinywani. Jamaa zao nao wakawaonyesha migongo. Chakula kikawa Cha maponeo na mara nyingi walilala udenda mkavu. Lakiniasiye na wake ana mungu Kwa kuwa masoomo yalikuwa bila malipo Mwaipusa alijipinda mgongo kama upinde Katika masomo yake Shida za nyumbani aliziacha kule . Na haikuwa ajabu alipoibuka Mwanafunzi bora wilayani kwani achanikaye kwenye mpini kwenye hafi njaa. Aliangukiwa Na bahati ya mtende akapata mfadhili. Akasoma katika shule ya upili pasipo masihara Kwa kuzingatia msemo , mzaha mzaha hutumbuka usaha. Miaka minee baadaye, Mwaipasa Alitamatisa masomo ya shule ya upili. Matokeo yalipotangazwa nyota yake sasa ilingaa Wilaya pekeebali katika nchi nzima. Akapata ari marudufu ya kusoma. Akasoma hadi chuo kikuu kwa msaada wa wafadhili Kampuni ainaaina zikawa zinahitaji utaalamu wake pindi tu alipotamatisha masomo ya Chuo kikuu .Akajiunga na benki kuu ya Kenya alikofanya kazi kwa bidii za mchwa kama Alivyoambia baba yake. Muda si muda vyeo na hadhi zikamfuata kule kazini . Mfuko yake Ikwa mizito .Yeye pamwe na wanuna wake wakapungia umaskini mkono. Utajiri ukawapa Mlalakakwa kwa mikono miwili. Jumba labda liitwe kasri akalijenga . Magari mazitomazito Yakamwandama. Nako kule nyumbani akakumbuka kutokako mema hurudi .Akawafadhili watoto wengine masskini kimasomo. Kwa hakika kisomo ndicho uti wwa mgongo maishani.

1. Msukumo wa Mwaipasa kusoma ulitokana na
A. Kutaka kujinasua kutoka katika umaskini
B. Kupasi mno katika umaskini
C. Mausia ya baba yake
D. Kufadhiliwa kusoma
2. Ni mbinu gani imetunika katika kifungu
Dhaifu kama utumbo wa samaki
A. Tashbihi
B. Methali
C. Tasfida
D. Sitiari
3. Mabebe yaliyomtoka akabaki gofu la mtu
Maneno haya yanamaanisha
A. Alinenepa
B. Hakutambulika
C. Alikuwa amekonda sana
D. Alibaki kwao
4. Nini maana ya jamaa zao wakawonyesha migongo
A. Waliwageuka wawaone mgongo
B. Waliwapa
C. Hawakuwapa hisani wala msaada
D. waliwakimu
5. Mama yake Mwaipusa
A. alikuwa mgonjwa mahututi
B. alikufa kutokana na ugonjwa uleule ambao ulimwandama baba
C. alikuwa ameenda katika safari isiyoeleweka
D. alikuwa akiteseka sana bila mtu kumsaidia
6. upi si wasia wa baba yake Mwaipusa
A. asijichunge na ugonjwa usio na dawa
B. awatunze ndugu zake wadogo
C. asidhamini utajiri kuliko elimu
D. elimu ndiyo itakayomwokoa kutoka katika
7. Walilalia udenda mkavu inamaanisha
A. walilala jamvi
B. walilala godoro
C. walikula hadi wakalala
D. walilala njaa
8. Methali gani haiwezi kulinganishwa na maisha ya Mwaipusa
A. Penye nia pana njia
B. Mbwa hafi maji aonapo ufuko
C. Kamba hukatika pabovu
D. Kikulacho ki nguoni mwako
9. Ni jambo gani Mwaipusa alifanya kuonyesha ukitendewa wema nawe tendea Wengine wema
A. Kununua magari makubwa
B. Kifanya kazi kwa bidii katika katika k[ampuni mbalimbali
C. Kuwatunza wanuna wake
D. Kuwafadhili wanuna wake
10. Ni kichwa kipi mwafaka kinachoshtahiki kifungu hiki?
A. Mwaipusa na ndugu zake
B. Wasia wa baba yake Mwaipusa
C. Kisomo kilivyomfaa Mwaipusa
D. Utajiri wa Mwaipusa

kiswahili revision papers