4.6. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Nne Sehemu ya Sita - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Aug 3, 2015, 9:46 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Mwangaza wa shamshi ulimrausha Ali che hiyo. Alifungua macho na Kuyakupakupa akajaribu kukumbuka alikokuwa gonezi ilipompaa. Alikumbuka na kutanabahi yote ya jana na zile hamaki zake. Hasira zile Na uchungu hazikupungua bilikuli. Aliondoka samadarini na kwenda mferiji Na baada ya kunawa Wajihi alimwangalia babu Yule wake ikiwa yupo Akaona amekwisha toka awali Alitoka nje akawaza na kuwazua aende baitini akachukue baadhi ya Labasi zake kabla ya kuteremka Pwani lakini akaona kuwa itambidi Alonge na waliomo ndani, pengine huenda wakaweza kumzuia. Aliamua
Aende mosi kwa mosi hadi forodhani. Huko alikuta kama desturi kuna ghasi nyingi baadhi ya vyombo
Vikitayarisha kwa safari mizigo ikipandishwa na kuteremshwa watu Wakisukumana huku na kule baharia na abiria wote wakishugulika Alizungukazunguka mpaka akamwona kijhulanga wahedi aliyemfahamu Ambaye wakati ule alikuwa katika hekaheka za kuangalia orodha Aliyoikamata mkononi. Alijongelea na kumwuliza ikiwa anamaizi Kama chombo chochote kingeondoka siku ile. Aliajibiwa “vyombo vingi vinondoka leo”. Ali alimweleza haja yake yakutaka Kujiandikisha katika chombo chochote kila kijana ule alimwangalia Kwa mastaajabu na Ali akafanya haraka kumweleza kuwa ana Safari muhimu na hana pesa siku hiyo.

1. Ni mwangaza wa nini uliomwamsha Ali?
a. Kurunzi
b. Jua
c. Karabai
d. kibatari
2. kwa nini Ali alikuwa akijaribu kutanabahi alikokuwa
a. alikuwa na usingizi wa pono
b. hakukuwa kumepambazu vizuri
c. mawazoye hayakuwa tulivu
d. bado kulikuwa na giza kizimwili
3. chumbani alimolala Ali palikuwa na nani?
a. Rafikiye
b. Abuye
c. Sahibuye
d. babuye
4. ni kauli ipi isyo kweli kulingana na habari
a. hakuchukuwa nguo zake
b. ali alilala kwake nyumbani
c. babuye alipondoka bila kumuaga
d. ali aliondoka baada ya babuye
5. kwa nini alitaka katu kwenda baitini
a. asisawishike vingine
b. hakuwa na nauli
c. alitaka kwenda pwani
d. asiweze kuwazuia wengine
6. ali aliamua kwenda wapi kulingana na aya ya pili
a. faraghani
b. pwani
c. bandarini
d. baitini
7. ni akina nani waliokuwa wakipakia na kupakuwa mizigo?
a. Makuli
b. Utingo
c. Baharia
d. abiria
8. kijulanga aliyepatikana na ali alikuwa orodha ya
a. vyombo
b. majina
c. vipuli
d. magari
9. kulingana na habari hii ali _____________
a. alifahamu chombo angeasafiria nacho
b. alikuwa mmoja wa kupandisha mizigo
c. alishikwa na kiwewe cha kusafirio baharini
d. hakufahamu hali ya uchukuzi baharini
10. jambo lililompa ali wasiwasi ni
a. mtutumko wa bahari
b. ghasia nyingi baharihi
c. kuadimikiwa na njenje
d. kukosa libasi

kiswahili revision papers